Header Ads

Matokeo Ya Marekani Live: Donald Trump 244, Clinton 209


Trump ashinda jimbo la Montana


Mgombea wa Republican Donald Trump ameshinda jimbo la Montana. Jimbo hilo lina kura 3 za wajumbe. Clinton sasa ana jumla ya kura 104 za wajumbe na Trump 140.

Trump 'ana nafasi nzuri' - New York Times


Gazeti la New York Times, ambalo limekuwa likiunga mkono Hillary Clinton, linasema mfumo wake wa kompyuta kwa sasa unabashiri uwezekano wa Trump kushinda kuwa 53%.

Louisiana kwenda kwa Trump


ABC News wanakadiria kwamba Donald Trump atashinda jimbo la Louisiana.
Jimbo hilo limepigia kura mgombea wa Republican katika chaguzi nne mtawalia lakini waliunga mkono  Bill Clinton mwaka 1992 na 1996.
Jimbo hilo huwa halichukuliwi kama ngome ya Republican kama yalivyo majimbo mengine jirani.Jimbo hilo lina kura nane za wajumbe.

Clinton mshindi Connecticut, kwa mujibu wa ABC


 Hillary Clinton ameshinda jimbo la Connecticut, ngome ya chama cha Democratic ambapo amejishindia kura saba za wajumbe, kwa mujibu wa ABC News. Clinton sasa ana kura za wajumbe 104 na Trump 129.

Trump mshindi jimbo la Arkansas


Trump anakadiriwa kushinda jimbo la Arkansas kwa mujibu wa ABC News. Jimbo hilo lina kura sita za wajumbe.
Kwa kura za wajumbe, sasa Trump ana 129 na Clinton 97

No comments