Header Ads

Dume Suruali Darasa Kwa Kizazi Cha DigitaliDume Suruali

Na John Joseph
WIMBO wa Dume Suruali ndiyo inawezekana ukawa msemo kwa Watanzania wengi kwa kipindi cha miezi kadhaa ijayo, hiyo ni kutokana na mashairi yaliyoandikwa na mtunzi wa wimbo huo, Mwana FA akimshirikisha V-Money.

Unazungumzia mwanaume anavyolalamika kulazimishwa kuhonga fedha kwa mwanamke. Mwan FA ambaye jina lake halisi ni bwana Hamisi Mwinjuma, amezungumza na gazeti hili kufafanua kile alichokiandika kwenye wimbo huo aliomshirikisha bi Vanessa Mdee:

Lengo lako hasa ni nini?
Ni kuwataka watu wasiwe wajinga kwa kuwa mapenzi ni hisia na siyo biashara. Matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara nyingi tu katika kizazi cha sasa. Sina maana ya kuwasema vibaya wanawake lakini tukumbuke hata upande wetu sisi wanaume kuna Malioo ambao wao wanapenda kuhongwa na wanawake, ujumbe huu ni maalum kwa pande zote.

Kwa nini Vanessa?
Vanessa ni aina ya wanawake ambao sisi wanaume tukimuona tunahisi ili umpate ni lazima umuhonge sana, sababu ya kumchagua yeye ni kwa kuwa anawakilisha vizuri wasichana wa aina hiyo ambao wengi wamekuwa na mitazamo hiyo.

Umetunga kwa kuwa yamekutokea?
Mimi ni msanii, nawakilisha mengi yanayotokea kwenye jamii, yapo yaliyonitokea na mengine watu wangu wa karibu na jamii kwa jumla, kuna vitu ambavyo unaongeza ili sanaa ikamilike lakini kwa ufupi nimezungumza ukweli.

Utunzi wa wimbo ulikuwaje?
Niliutunga ndani ya muda wa siku moja niliyoenda studio lakini ilinichukua mwezi mzima kuwa naurekebisha hapa na pale. Hata Vanessa nilipomweleza alikubaliana na wazo langu na kuamini utafanya vizuri.

Kwa nini ulichagua MJ Records?
Prodyuza wa wimbo huo ni Daxo Chali ambaye ni mdogo wake Marco Chali. Nilienda MJ kwa Marco nikamueleza nataka kazi fulani akanipa ‘beat’ mbili, nikachagua yangu na Vanessa naye akachagua hii ambayo ndiyo imetumika kwenye wimbo.
Tuliamua kuchagua hiyo kwa kuwa Vanessa alinishauri ni beat laini ambayo kwanza itakuwa na ladha tofauti ndiyo maana tukaitumia.

Umemtaja tajiri Salah kwenye wimbo, ni nani?
Huyu ni rafiki yangu wa karibu, ni mmoja wa watu wangu ambaye amekuwa anashangaa sana jinsi wanaume wanavyohonga.


Mashairi ya Dume Suruali

Mwana FA
Hudat hudat hii ni salam na ufahamu
Kama unauza mapenzi siyo kwa binamu
Huna haja ya kusubiri hii ni hukumu
Hakuna kitu utapata utangoja kama askari wa zamu
Dume suruali dume kaptula
Shauri zako ilimradi sipati hasara
Usione utani me sihongi hata kwa ishara
Utaniambia nini mpaka unigeuze fala
Kwanza nasikia hongo zinaleta mkosi
Sentano yangu hugusi hata ukiongea kidosi
Yabaki mapenzi tusileteane ujambazi
Hata upige sarakasi utachonga viazi.

BAHILI KAMA NINI!!!!!!!!! Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada!
Hunitakii mema.

Kiitikio
We dume suruali kaa mbali nami
Kama dume suruali kaa mbali nami
Huendani na mimi
I want Gucci, Fendi, spend it on the girl like me
My name is Vee Money, money spend on the girl like me

MWANA FA
Nihonge nanunua nini kwa nini yaani!
Kuna kipi nisichokijua ina TV ndani?
Usiulize n’takupa nini dada piga moyo konde
Viuno vingi kama mwali wa kimakonde
Usipende hela kama mfuko
Au fanya unavyofanya upate zako
Vishawishi vingi binti sema na moyo wako
Na ujifunze pesa zinauza utu wako
Tajiri mtata kama Salah
Zipo ila sitoi me ni balaa
Unapenda hela zangu nami nazipenda pia
Kila mtu abaki na zake bye baby tutaongea

MWANAUME WA HIVYO WA NINI SASA!!!!! Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema


Vanessa
Aje aje ajeeee me mtoto fulani ghali
Nihonge gari Ma sweet sweet baby
Wanna see you today unipeleke party
Aje aje ajeee njoo nikupe TBT

MWANA FA
Siyo kwa enzi ya Magufuli
Zali ilikuwa long siku hizi hakuna la mentali
Nikikuhonga na ukiniacha nitakujia usingizini
Naepusha shari matatizo yote ya nini
Hakuna kipya chini ya jua
Hata nisiyoyafanya nishayasikia
Ningekuwa mhongaji ningeshafulia wangu
Mademu wangu wa zamani wote wangekuwa maadui zangu
MWANAUME HOVYO WEWE!!!!! Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema

Vanessa
Baki na hamu zako

Kiitikio

VANESSA
Baba bure huyuu!!!

Mwana FA
Hata pantoni lina staff

Vanessa
Unamwambia nani sasa! Unamwaaambia nani sasa!

No comments