Header Ads

Hayawi Hayawi Kocha Lwandamina Atambulishwa Rasmi Yanga SC

 DAR ES SALAAM: HAYAWI HAYAWI YAMEKUWA; Kocha mpya wa Klabu ya Yanga, George Lwandamina ametua kikosini hapo na kukabidhiwa jukumu la kuinoa klabu hiyo akichukua nafasi ya Mholanzi, Hans Van der Pluijm aliyepewa jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi.
lwandamina-6Kocha Mpya wa Klabu ya Yanga, George Lwandamina akizungumza na wanahabari.
Lwandamina ambaye ni raia wa Zambia ametambulishwa leo rasmi na Makamu wa Rais wa Yanga, Clement Sanga mbele ya waandishi wa habari.


“Tunaamini kocha atatusaidia kutoka hapa tulipofikia na kusonga mbele hasa katika michuano ya kimataifa,” amesema Clement Sanga.
Lwandamina atakuwa akifanya kazi na Hans van der Pluijm ambaye sasa ni mkurugenzi wa ufundi la kbalu hiyo. Pluijm ambaye amepanda cheo, aliifikisha Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.
 Awali Yanga hawakutaka kumzungumzia kocha huyo. Baada ya kutambulishwa rasmi, Kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina amesema atapambana vilivyo kuhakikisha anafanya vema.
 Hans van der Pluijm akizungumza na wanahabari.
Lakini Lwandamina, amekiri kuwa kweli ni jukumu gumu kwake kama changamoto.“Lakini nitapambana kufanya vizuri, najua ni changamoto mpya kwangu lakini nitafanya kila linalowezekana,” alisema.
 
Lwandamina akijibu maswali ya wanahabari.
Lwandamina ameomba Wanayanga kumpa ushirikiano ili kufikia malengo yake. Lakini amesisitiza suala la ushrikiano ni namba moja kwake.

No comments