Header Ads

Instagram, WhatApp na Facebook Zakua kwa kasi

Mitandao ya kijamii inayomilikiwa na tajiri namba sita duniani mwenye utajiri wa Dola za Marekani bilioni 52.2  ambazo ni  sawa na Shilingi trilioni 114 za Tanzania, Mark Zuckerberg (32), inaonyesha kukua kwa kasi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Novemba 2 mwaka huu iliyotolewa kupitia ukurasa wa Facebook wa Mark Zuckerberg, inaonyesha mtandao wa Facebook umekua na kufikia watu bilioni 1.8, ambapo Whatsap imefikia  bilioni 1, Facebook Messenger bilioni moja na Instagram milioni 500.


Watumiaji wa mitandao hiyo wamekuwa wakipendelea kuangalia vipande vya video na ku-‘share’ kila siku.
Malengo ya mitandao hiyo ni kuongeza idadi zaidi ya watu wanayoitumia na kila siku wanaendelea kuiboresha kila siku.

No comments