• Latest News

  November 18, 2016

  JPM Aikosa Tuzo ya Person of the Year 2016 Inayotolewa na Forbes

   Madonsela.
  Aliyekuwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali na Wakili nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela jana ametangazwa kuwa ndiye mshindi  wa Tuzo ya Mtu Mashuhuri Afrika ya Forbes (Person of the Year #POY2016).

  Tuzo huyo hupewa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuiinua jamii kwenye njanja mbalimbali za maisha kama vile uchumi, siasa, utamaduni.

  Katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo, Thuli Madonsela alikuwa akichuana na Michiel Le Roux kutoka Afrika Kusini, Rais wa Mauritania, Ameenah Gurib, Jamii ya watu wa Rwanda na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
  Mwaka 2015 tuzo hii ilikwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya MeTL, Mohammed Dewji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JPM Aikosa Tuzo ya Person of the Year 2016 Inayotolewa na Forbes Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top