Header Ads

KIPYA MPYA MGHANA ATUA DAR ES SALAAM KUJIUNGA NA SIMBA

Baada ya awali kuonyesha nia ya kuhitaji kipa mpya, hatimaye kipa Daniel Agyei amewasili rasmi nchini tayari kujiunga na kikosi cha Simba.

Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar, kipa huyo alipokelewa na Mratibu wa Simba, Abbas Ally. 
Simba itafanya mazungumzo na kipa huyo raia wa Ghana ambaye pia ni kipa namba moja wa kikosi cha Medeama cha Ghana lengo ni kuongeza ushindani kwenye nafasi hiyo.

"Ndiye anaonekana kuwa chaguo sahihi, kazi yake ilionekana akiwa kwenye Kombe la Shirikisho," kilieleza chanzo.

Kocha Joseph Omog alipendekeza kuongezwa kwa kipa mmoja ili ‘kumbusti’ Vicent Angban.

No comments