Header Ads

Maalim Seif Amezuiliwa Na Jeshi La Polisi Kufanya Mkutano wa Ndani Mtwara

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, leo alialikwa kuhudhuria mkutano wa ndani wa chama ulioandaliwa na Jumuiya ya Vijana ya CUF(JUVICUF) Mtwara Mjini, kama mgeni rasmi. Kwa taarifa za uhakika ni kuwa Jeshi la Polisi wadaiwa kuipokea barua ya Jumuiya ya Vijana ya CUF(JUVICUF ) na kuijibu wakiruhusu Mkutano huo uendelee na kwamba wangeulinda. Jana, Polisi pia walikabidhiwa barua ya Katibu Mkuu wa CUF kwenda kwa IGP na ma RPC Lindi na Mtwara akiwajulisha juu ya ziara yake.
Mapema leo wakati Maalim Seif akitua Mtwara Mjini , Polisi wamekwenda na magari yao na vitambaa vyekundu na kuzingira ukumbi wa kikao huku watu wakifukuzwa. Kisha Polisi wakawapa viongozi wa CUF barua nyingine ya kutengua ile barua ya ruhusa.

No comments