Header Ads

Mbowe Amtwanga Swali Waziri Mkuu Kuhusu Rushwa kwa Wabunge wa CCM, Naibu Spika Azuia Lisijibiwe
DODOMA: Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu leo amedai kuwa, mnamo siku ya Jumanne tarehe 25/10/2016 saa mbili usiku kiliitishwa kikao cha wabunge wa CCM ambacho Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa Mwenyekiti, na kilihudhuriwa na Katibu MKuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwa ajili ya kujadili Muswada wa Habari.
 
Mbowe amesema kuwa Wabunge wakiwemo Mawaziri walihongwa shilingi milioni 10 kila mmoja ili waweze kusaidia kupitisha Muswada wa Habari unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni kesho.

Lakini Naibu spika amekataa katakata Waziri mkuu kujibu swali la Mbowe kwa waziri mkuu kuhusu tuhuma hizo za wabunge wa CCM kuitwa kwenye kikao na kupewa fedha kiasi cha milioni 10 kila mmoja ili wasiibane serikali kwenye muswada wa sheria unaowasilishwa kesho

Maelezo ya Naibu spika ni kuwa swali hilo halihusu sera, huku Mbowe akidai linahusu sera kwa kuwa ni rushwa kwa wabunge.

No comments