Header Ads

MISS KILIMANJARO, 2016 ATEULIWA KUWA BALOZI WA PII

 Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa PII, Amos Oyomba akimkabidhi Miss Kilimanjaro mwaka 2016, Glory Msuya hundi ya shilingi milioni moja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo, Ebenezer Msuya.

Miss Glory alizungumza na wanahabari hawapo pichani. Kulia kwake ni Oyombo

 Kampuni ya Perfect Infotech International Limited(PII Limited)ya Mikocheni jijini Dara, leo imemteuwa Miss Kilimanjaro mwaka 2016, Glory Minja kuwa balozi wa kampuni hiyo.

PII Limited ambayo inatoa mhuduma ya usimamizi na ulinzi wa magari, mtu binafisi, ofisi na  makampuni mbalimbali, imemteuwa Glory kwa sababu anaweza kuitangaza vyema huduma hiyo kutokana na vigezo vyake alivyonavyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa PII, Ebenezer Msuya alisema kampuni yake imejipanga vyema katika kutoa huduma hiyo ya usimamizi na ulinzi wa vitu mbalimbali vya kazini na majumbani pamoja na mtu mwenyewe na itashirikiana na Miss Glory katika mambo mawili, kijamii na kimasoko.

Hata hivo Glory ambaye alikuwa mshiriki mwenye namba 18 amejipanga vyema kuisaidia jamii katika suala la familia na usalama.

“Ni muda saa wa Watanzania kubadilia na kuweka ulinzi katika maliz zetu, kwa mfano PII inaweza kufunga na kufuatilia mwenendo mzima wa gari linalomchukua mwanao kila siku kwenda shule, ofisini, kwenye kampuni na hata mtu binafsi kwa kutumia teknolojia ya kisasa,”alisema Glory.

No comments