• Latest News

  November 11, 2016

  MSANII WILDAD KUTOKA THE INDUSTRY KAACHIA WIMBO MPYA MKITONI


  Lebo ya The Industry iliyo chini ya umiliki wa kundi la Navykenzo yaachia ngoma nyingine ya msanii wao Wildad iitwayo "Get It On". Wimbo unapatikana Mkito na unaupata kwa kubofya link hii: http://bit.ly/GetITOn


  Msanii huyo wa RnB amekuja kuteka mioyo ya kina dada kwa muonekano na sauti yake ambayo ni kivutio kikubwa katika kuimba kwake. Akizungumza mara baada ya kuachia wimbo huo kwenye ofisi za Mkito, Masaki jijini Dar Wildad amesema “Nimekuja kuleta ladha mpya ya RnB na kipaji changu ni cha kipekee na lengo kubwa la ni kuvuka mipaka”.

  Wildad alijiunga na “The Industry” May mwaka huu wa 2016 na ngoma yake pamoja na video vinaashiria kuwa ana matarajio makubwa ya kuifikisha RnB ya Tanzania kwenye matawi ya juu.

  Itazame hapa video yake ya “Get It On” kisha pakua Mkito hapa http://bit.ly/GetITOn

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MSANII WILDAD KUTOKA THE INDUSTRY KAACHIA WIMBO MPYA MKITONI Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top