Header Ads

Muhimbili yakusanya Sh. bilioni 4.6

 Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano ya umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaesha akizungumza na wanahabari
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeongeza mapato yake kwa asilimia 100 baada ya kukusanya jumla ya shilingi bilioni 4.6 ukilinganisha mwaka jana ambapo walikusanya sh. Bilioni 2.3.
Taarifa  iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika hospitali hiyo, Aminiel Aligeisha imesema:
“Baada ya kuongeza kasi ya usimamizi wa wafanyakazi na kupunguza kero za weafanyakazi, hospitali imeongeza uzalishaji wenye tija kwa kiwango kikubwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa kuanzia Desemba 2015 hadi Oktoba 2016 hospitali ilizalisha wastani wa kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kwa mwezi kutoka wastani wa shilingi bilioni 2.3 iliyokuwa ikizalishwa kwa kipindi kama hicho cha Desemba 2014 hadi Oktoba 2015.”
Alisema hayo ni mafanikio makubwa  kwa upande wa mapato kuwahi kupatikana katikakipindi kifupi sana cha miezi miwili tu.
Aliongeza kuwa hospitali kwa sasa kulingana na uzalishaji unaoonekana, inajitahidi kupunguza madeni iliyonayo kwa wazabuni mbalimbali wakiwemo wanaoanyia matengenezo kinga ya vifaa tiba vya hospitali.
Kuhusu upatikanaji wa dawa, Aligaesha alisema kwa sasa wagonjwa wanapata dawa kwa zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa  ya hospitali na tiba kwa wagonjwa wanaofanyiwa kliniki inaanza saa tatu asubihi.

No comments