Header Ads

Mwili wa Samuel Sitta Kuwasili Alhamisi, Kuzikwa Urambo Jumamosi

Msanii Ummy Wencelaus ‘Dokii’  akisaini kitabu cha waombolezaji.

 Kiongozi Mkuu wa Kitaifa wa Skauti ambaye pia alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantuma Mahiza akisaini kitabu cha maombolezo.

DAR ES SALAAM:  Viongozi  mbalimbali wa kitaifa wamezidi kumiminika nyumbani kwa aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel John Sitta maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam.

Sitta alifariki dunia usiku wa kuamkia jana  saa 10.50 alfajiri kwa saa za Tanzania  wakati akipatiwa matibabu ya saratani ya tezi dume katika Hospitali ya Technical University of Munuch nchini Ujerumani.

Tovuti hii imetua tena nyumbani kwa marehemu mapema leo asubuhi maeneo ya Masaki, jijini Dar es Salaam na kushuhudia viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikiali wakifika kuwafariji wafiwa.

Viongozi hao ni pamoja na Kiongozi Mkuu wa Kitaifa wa Skauti ambaye pia alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantuma Mahiza, aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Kahama James Lembeli.

Ratiba

Akizungumza na tovuti hii, mmoja wa wanakamati wa msiba huo aitwaye Gerald Mongela ametoa ratiba ya msiba kama ifuatavyo;

Mwili wa Marehemu Samuel Sitta utawasili Alhamisi ya Novemba 10, mwaka huu na kulala nyumbani kwake Masaki jijini Dar.

Ijumaa Novemba 11, 2016 mwili wa marehemu utatolewa asubuhi nyumbani kwake kuelekea Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa pamoja na misa.

Saa tisa alasiri Ijumaa mwili utapelekwa Dodoma kwa ajili ya heshima za mwisho za kibunge na baada ya zoezi hilo utasafirishwa kuelekea Urambo mkoani Tabora.

Jumamosi Novemba 12, mwili utaagwa na wakazi wa Urambo kisha kuzikwa siku hiyohiyo

No comments