Header Ads

Orodha ya vyuo 26 vilivyofutiwa usajili na NACTE leo

 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26 kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika cheti cha usajili wa vyuo hivyo, huku likisimamsisha utoaji wa programu zilizokuwa zikitolewa katika vyuo 20 ambazo hazijasajiliwa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo.

Katibu huyo amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi huo, wamebaini vyuo 26 vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika cheti cha usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika,wakati vyuo viwili vikiwa na vituo vya satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika.

NACTE ni bodi iliyoanzishwa kisheria chini ya Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, kifungu cha 129, kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo nchini Tanzania.  Chini ya sheria hiyo, ili kufikia na kudumisha hali ya mtoa mafunzo, vyuo vyote vinatakiwa viwe vimesajiliwa, vibali na kuwa mitaala iliyopitishwa na baraza. Vyuo haviruhusiwi kuanza kutoa kuanza kutoa huduma yoyote ya mafunzo bila idhini ya baraza.

Hapa chini ni mgwanyo wa vyuo katika makundi matatu na hatua zilizochokuliwa dhidi ya kila kundi

Jedwali 1: Vyuo vya Ufundi vilivyofutiwa usajili
S/N     CHUO
1     Institute of Management and Development Studies – Iringa
2     Green Hill Institute – Mbeya
3     Institute of Business and Social Studies – Mbeya
4     Loyal College of Africa – Mbeya
5     Mbeya Training College – Mbeya
6     Mbengwenya College of Business and Information Technology –Mbinga
7     New Focus College – Mbeya
8     Shukrani International College of Business and Administration –  Mbeya
9     Majority Teachers College – Mbeya
10     Rukwa College of Health Sciences – Sumbawanga
11     MAM Institute of Education – Mbeya
12     Belvedere Business and Technology College – Mwanza
13     Geita Medical Laboratory Sciences and Nursing Training College – Geita
14     Global Community College – Geita
15     Muleba Academy Institute – Muleba
16     St. Bernard Health Training Institute – Katoro, Geita
17     Victoria Institute of Tourism and Hotel Management – Mwanza
18     Gisan Institute of Health Sciences – Mwanza
19     Dar es Salaam Institute of Business Management – Dar es Salaam
20     SAMFELIS College of Business Studies – Dar es Salaam
21     Ellys Institute of Technology – Bunda, Mara
22     Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators – Arusha
23     Emmanuel Community College – Kibaha
24     Modern Commercial Institute – Dar es Salaam
25     Marian College of Law – Dar es Salaam
Jedwali 2: Vyuo vya Ufundi vinavyotoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa
S/N     CHUO     MAFUNZO
1     MISO Teachers College – Mafinga     Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education
2     Tusaale Teachers College – Mafinga     Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education
3     The St. Joseph’s College Institute of Business and Management (SJCIBM) – Morogoro    
4     The Golden Training Institute – Dar es Salaam    
5     Nkrumah Mkoka Teachers College – Kongwa, Dodoma    
6     National Institute of Agriculture (Chuo cha Kilimo cha Taifa) – Arusha    
7     Musoma Utalii Training College – Musoma    
8     Mwanza Polytechnic Institute – Mwanza    
9     Mwanza Polytechnic Institute – Maswa    
10     Ruter Institute of Financial Management – Mwanza    
11     Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Mwanza    
12     Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Geita    
13     Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Bukoba    
14     Singni International Training Institute – Bukoba    
15     Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Kahama    
16     Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Simiyu    
17     Richrise Teachers College – Geita    
18     Twiga Training Institute – Musoma    
19     Zoom Polytechnic Institute – Bukoba    
20     St. Thomas Training College – Shinyanga    
Jedwali 3: Vyuo vya Ufundi vyenye Vituo vya Satellite / Kampasi
S/N     CHUO
1     MISO Teachers College – Mafinga
2     Rungemba Teachers College – Mafinga

No comments