• Latest News

  November 04, 2016

  Rais Magufuli kufanya mahojiano na waandishi wa habari LEO


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 04 Novemba, 2016 atafanya mahojiano ya kwanza na waandishi wa habari tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.
   
  Mahojiano haya yatarushwa moja kwa moja na vituo vya habari vya redio na televisheni kutoka ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na yataanza saa 4:00 asubuhi.
   
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inapenda kuwaalika wananchi wote kusikiliza na kutazama mahojiano hayo ili mpate fursa ya kujua mambo mbalimbali ambayo Mheshimiwa Rais atayatolea majibu. 
   
  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli kufanya mahojiano na waandishi wa habari LEO Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top