Header Ads

Rais wa Zamani wa Cuba, Fidel Castro Afariki Dunia akiwa na miaka 90


HAVANA, CUBA: Rais wa zamani wa Cuba, na kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha nchini humo, Fidel Alejandro Castro Ruz amefariki dunia alfajiri ya leo Novemba 26, 2016 akiwa na umri wa miaka 90.

Cuba's President Raul Castro attends an event marking the 1953 assault on the Moncada military barracks in Holguin, Cuba, July 26, 2009. REUTERS/Enrique De La Osa (CUBA POLITICS ANNIVERSARY)Raul Castro.

Kifo cha Castro aliyezaliwa August 13, 1926 kimetangazwa kwenye Televisheni ya Taifa na Rais wa sasa wa nchi hiyo ambaye ni mdogo wa marehemu, Raul Castro.

castro-1Rais wa zamani wa Cuba, Fidel Alejandro Castro Ruz.

Castro alichukua madaraka ya nchi hiyo baada ya kufanya mapinduzi mnamo mwaka 1959 na kuiongoza Cuba kwa miaka 49, kabla ya kuachia ngazi February 2008 na kumkabidhi uongozi mdogo wake, Raul Castro kufuatia kuugua kwa muda mrefu.

nyerere-na-castroMwalimu Nyerere akimkaribisha Fidel Castro Tanzania, Jumanne Machi 22, 1977. Castro amefariki dunia leo huko Havana akiwa na miaka 90.

Miaka miwili kabla, mdogo wake , Raul alishikila madaraka ya kaka yake wakati kaka yake alipofanyiwa upasuaji wa dharula wa utumbo mpana.

Baada ya Malkia Elizabeth II na Mfalme wa Thailand, kiongozi huyo wa Cuba ni wa tatu duniani kwa kukaa madarakani kwa muda murefu zaidi.

Wafuasi wake wamekuwa wakiamini kuwa, Castro ndiye aliyeirudisha Cuba kwa wananchi wake huku wapinzani wakipinga uongozi wake wa kimabavu.

castro-2Mambo ya Kumkumbuka Fidel Castro

1926: Alizaliwa Kusini Mashariki mwa Jimbo la Oriente, Cuba

1953: Alifungwa jela baada ya kuanzisha upinzani na uongozi wa Batista

1955: Aliachiliwa huru kutoka gerezani.

1956: Akiwa na Che Guevara, alianzisha vita kuipinga serikali ya nchi hiyo.

1959: Aliushinda utawala wa Batista, na kuapishwa kuwa Waziri Mkuu wa Cuba

1960: Alipigana na CIA kutokana na wananchi wake waliokuwa uhamishoni.

1962: Aanzisha mpango wa utengenezwaji wa vinu vya nuclear.

1976: Alichaguliwa kuwa rais wa Bunge la Cuba.

1992: Aliingia makubaliano na Marekani kuhusu wakimbizi wa Cuba.

2008: Aliachia madaraka ya urais wa nchi hiyo na kumkabidhi mdogo wake Raul Castro.

CHANZO: BBC NEWS

No comments