• Latest News

  November 02, 2016

  SAFARI YA MWISHO YA SIMBA ASIYEFUGIKA, BURIANI THOMAS MASHALI  Kila mwanadamu ataonja mauti, kila mwanadamu ana safari yake ya mwisho.

  Safari ya mwisho ya bondia Thomas Mashali ilikuwa leo alipozikwa kwenye makabuli ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Mashali alifariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

  Hadi anafariki dunia, Mashali alikuwa ni bondia namba mbili kwa viwango baada ya Francis Cheka lakini ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kumtwanga Cheka.

  Alikuwa na mikanda minne ya ubingwa katika mashirikisho mbalimbali likiwemo lile la UBO.


  Mashabiki wengi walijitokeza leo kumuaga kwenye Viwanja vya Leaders kabla ya kumzika kwenye makaburi hayo ya Kinondoni.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SAFARI YA MWISHO YA SIMBA ASIYEFUGIKA, BURIANI THOMAS MASHALI Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top