Header Ads

Sakata la Wema na Muna, Mama Wema aingilia kati! Adai Wema hawezi fanikiwa bila Muna! (Video ipo hapa)

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii na hasa Instagram na umefollow pages tofauti tofauti za mambo ya udaku naamini utakuwa unalifahamu hili linalo endelea sasa hivi kwenye mitandao hiyo kumuhusu staa wa movie Wema Sepetu pamoja na rafiki yake Muna Love.


Inasemekana kuwa wawili hao hawana mahusiano mazuri kwasasa kama ilivyo zoeleka urafiki wao kunoga kinoma noma hapo awali. Ni kutokana na kinachosemekana kuwa ni imani za kishirikina ndio zimesababisha wawili hao kutofautiana. Kutokana na kinachosemekana kwamba eti Muna Love anataka kuchukua nyota ya Wema Sepetu.

Soudy Brown amepiga story na Wema Sepetu na mwanadada huyo amekanusha kabisa kuwa na utofauti na rafiki yake huyo kipenzi.

Lakini Soudy Brown hakuishia hapo tu, aliinyaka voice note ya mama mzazi wa Wema Sepetu akifunguka kila kitu kuhusiana na sakata hilo la wanae hao wawili (Wema na Muna).

Wanasemaga mjini cha bure salamu tu, au vipi eeh? Sasa huo msemo kwetu mimi na wewe wala hauna nafasi, kwasababu nimekukusanyia ubuyu kamili hapa chini kwenye video hii bureeee. Kazi kwako tu kubofya play.

No comments