• Latest News

  November 21, 2016

  TARIMBA NAYE AMLILIA SHELUKINDO, ASEMA ALIKUWA KIONGOZI SHUPAVU  ABBAS TARIMBA

  Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Abbas Tarimba ameeleza majonzi yake kuhusiana na kifo cha aliyekuwa makamu wake, Isaac Shekiondo.
  Shekiondo aliyekuwa maarufu kama Clinton amefariki dunia leo katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.
  Tarimba ambaye alikuwa mwenyekiti na Clinton akiwa makamu, amesema alikuwa kiongozi shupavu na mwenye utayari wa kujitolea.
  “Mimi na akina Shekiondo tulifanya kazi nzuri, nilimjulia Yanga lakini alijitoa na kujitolea,” alisema.
  “Katika masuala ya kutofautiana na hoja, ilikuwa inatokea wakati mwingine tunapishana lakini lengo lilikuwa ni kupata Yanga yenye matumaini na umoja.”
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TARIMBA NAYE AMLILIA SHELUKINDO, ASEMA ALIKUWA KIONGOZI SHUPAVU Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top