Header Ads

TB Joshua Atabiri Clinton Kushinda Urais wa Marekani Leo

Muhubiri maarufu nchini Nigeria, TB Joshua (pichani) amesema ametabiri kuwa mgombea kutoka chama cha Democtratic nchini Marekani, Hillary Clinton atamshinda Donald Trump wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wenye ushindani mkali leo Novemba 8, mwaka huu.
Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook, TB Joshua amesema kuwa Bi. Clinton atashinda kwa ushindi mdogo, lakini atakabiliwa na changamoto nyingi – likiwemo jaribio la kupiga kura ya kutokuwa na imani dhidi yake.
“Boti ya rais mpya itakuwa imefungwa,” aliongeza TB.
TB Joshua ni mmoja wa viongozi wa kidini wenye ushawishi na utata barani Afrika, huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa utabiri wake ni wa uhakika.

No comments