Header Ads

Usiku Wa Mastaa Si Wa Kukosa Maisha Basement Jumapili Hii

 
 Staa wa Bongo Fleva, Pam D.
Lulu Diva.
 
 
MASTAA kibao wa Muziki wa Bongo Fleva wakiongozwa na Mesen Selekta, Pam D, Tunda Man, Country Boy, TID, Sold ground family, Bob Junior na Haitham wanatarajiwa kukutana siku ya Jumapili uso kwa uso na mastaa wa filamu wakiongozwa na Kajala ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar.
Akizungumza na Showbiz Xtra, mratibu wa shoo hiyo, Geofrey Jilla ‘Jilla the Boss’ alisema kuwa, mbali na uwepo wa wakali hao, mashabiki wa burudani wategemee kupiga picha ‘red carpet’ na mastaa mbalimbali.
“Shoo hii pia itawapa fursa wale wote waliozaliwa mwezi wa 11 kukata keki ya pamoja na mastaa mbalimbali. Tutakuwa na mamodo wote Bongo wakiongozwa na Kidoa, Lulu Diva, Amber Lulu, Erycah na wengine kibao kwa mtonyo wa 10,000 tu,” alisema Jilla.

No comments