Header Ads

Wanasayansi Udsm Wafurahia Kuhitimu

WANACHUO wa kitengo cha sayansi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mapema leo wameonekana wakifurahia kuhitimu masomo yao ambapo kamera yetu imewashuhudia wakipiga picha mbalimbali chuoni hapo kabla ya kuelekea kwenye Ukumbi wa Mlimani City, kulipofanyika sherehe za mahafari ya 46 ya chuo hicho.
Mmoja wa wahitimu hao aliyejitambulisha kwa jina la Dauson Amos akizungumza na mtandao huu alisema, anamshukuru Mungu kwa kuweza kuhitimu masomo yake hayo ya sayansi.
Mbali na mahafari hayo kwa wanasayansi, mahafari mengine kwa ajili ya kozi nyingine chuoni hapo yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

No comments