• Latest News

  November 13, 2016

  YAMETIMIA, JOSE MOURINHO AANDAA DAU LA KUMNG'OA OZIL ARSENAL, MSHAHARA WAKE HUU HAPA


  Kocha Jose Mourinho amekubali kumwaga kitita cha euro milioni 15 ili kwa kiungo Mesut Ozil (28) ili atue Old Trafford na kujiunga na Man United.

  Mourinho ambaye aliwahi kufanya kazi na Ozil wakiwa Real Madrid, yuko tayari kumwaga kitita hicho ili kumnasa Ozil raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki ambaye ni tegemeo kubwa katika kikosi cha Arsenal ya mzee Arsene Wenger.

  Taarifa za ndani kutoka Manchester United, zimeeleza, Mourinho anaamini hiyo ni ofa bora kumpa Ozil na kila kitu kitakwenda vizuri kama Mjerumani huyo, hataingia mkataba mpya na Arsenal.

  Kuhusiana na mshahara imeelezwa itakuwa ni euro 290,000 euro kwa wiki kwa kuwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal.

  Taarifa za awali zimeeleza kwamba Arsenal kama wataongeza naye mkataba walikuwa tayari kumlipa euro 185 kwa wiki, ikiwa wameongeza euro 20,000 kwa kila wiki, yaani euro 80,000 kwa mwezi zikiwa ni sehemu hiyo ya nyongeza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: YAMETIMIA, JOSE MOURINHO AANDAA DAU LA KUMNG'OA OZIL ARSENAL, MSHAHARA WAKE HUU HAPA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top