• Latest News

  November 02, 2016

  Zuku Swahili Movies Kuwanufaisha Wasanii Bongo

  Abuu Kimario, Afisa Mahusiano Bodi ya Filamu Nchini akizungumza jambo.

  Kushoto ni Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania, Omari Zuberi (katikati).
  Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) Saimon Mwakifamba akizungumza jambo.


  Baadhi ya wadau na wasanii wakifuatilia uzinduzi huo.

  Kampuni ya Visembuzi aina ya Zuku leo imezindua rasmi chanel yake ya Zuku Swahili Movies ambayop itakuwa ikionyesha kwa wingi kazi za sanaa za kitanzania kwa lengo la kukuza Kiswahili, kazi za kitanzania na kuwafikia watazamaji wengi wa Afrika Mashariki na nchi zingine zinazotumia Lugha ya Kiswahili.

  Akizungumza mbele ya wanahabari,  Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania, Omari Zuberi amesema kuwa kutokana na fursa ya ukuaji wa Bongowood,  Zuku TV iliwekeza na kuzindua Zuku Swahili Movies mwaka 2013, ili kukuza sekta ya filamu Tanzania lakini awamu hii wameboresha kwa kuzipa nafasi zaidi filamu za Kiswahili. 

  “Mwaka 2013 tulianzisha Zuku Swahili Movies ikiwa ina vitu vingi lakini awamu hii  kupitia chaneli ya 210 utapata kuburudika kwa filamu za kiswahili ambazo nyingi zikiwa zinatoka katika kiwanda cha Bongo Movies,’’alisema Zuberi.

  Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) Saimon Mwakifamba amewataka Zuku kuboresha maslahi zaidi kwa wasanii na waandaaji wa filamu na siyo madalali. Wasanii wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni Chichi, JB, Emmanuel Myamba na wengineo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Zuku Swahili Movies Kuwanufaisha Wasanii Bongo Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top