Header Ads

Nisha Amchana Nay wa Mitego Kisa Mimba


MSANII wa filamu za vichekesho nchini, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kumchana staa wa Hip hop, Nay wa Mitego aliyewahi kuwa mpenzi wake akifunguka kuwa hajawahi kusema kuwa ana mimba ya staa huyo anayehit na ngoma yake ya Pale Kati Patamu.

Nisha ameamua kumchana Nay baada ya mwana Hip hop huyo kukanusha kuwa amempa mimba mwanamama huyo akidai kuwa hajaonana naye kwa takribani miaka mitatu kupitia kipindi cha U-Heard cha Clouds FM ambapo alinukuliwa akisema; “Mimi sielewi nimeshirikishwaje kwenye suala la mimba, tena naambiwa nimembaka, hivi mimi ninavyogombaniwa na wanawake naanzaje kumbaka?.”


Kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram, Nisha amefunguka haya akimchana Nay na kutupia picha yake iliyounganishwa na post ya Siwema_255 ambaye naye alikuwa anamponda Nay na kumfariji Nisha;

#Naywamitego iko hivi kabla hujaandika kitu chunguza sio unakurupuka tu na kuandika ujinga. ulinisikia na kuniona wapi nimekutaja kwamba wewe ndo baby dady wangu???? hivi naanzaje kuzaa na wewe Nay?? kifupi pamoja na mapungufu na makosa yaliyojitokeza kwa baba k wangu humfikii hata kwa kucha labda umemshinda hizo tatoo zako kama bibi harusi.


Nikuombe msamaha kwa kipi acha kudandia treni kwa mbele.??? tena watishe hao hao WANAUME SURUALI mimi simuogopi yeyote anayekojoa akiwa amesimama wala amechutama.

tena USINICHOKONOE

nb:chanzo chako cha kutagiwa labda nikufunue akili yako ni hiyo coment huyo ni mimi???? nna mahusiano naye??.. next time tumia akili.

#NASEMA# HIVIIIII #SIMUOGOPI #MTU YETOTE…..

Ujumbe wenyewe huu hapa;

No comments