Header Ads

Amanda Ampigia Chapuo Jokate kwa ‘Mapouda’

Staa wa Bongo Muvi, Tamrinah Poshi ‘Amanda’ .

DAR ES SALAAM: Staa wa Bongo Muvi, Tamrinah Poshi ‘Amanda’ ameweka wazi kuwa anamkubali kinomanoma Mwanamitindo Jokate Mwegelo kwa sababu anaweza kuingia kitaa hata kama hajajipodoa na bado muonekano wake ukawa bomba tofauti na wasanii wengine.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo.
Amanda aliiambia 3 Tamu kuwa, wasanii wengi hawawezi kuonekana machoni pa wengi kama hawajapaka make-up ila Jokate ni tofauti.
“Unajua Jokate ni miongoni mwa wasanii wachache wenye muonekano wa asili hata kama hajapaka mapouda, anaingia kitaa kama kawa na anaonekana bomba tu, hata mimi ni hivyo hivyo. Ila kuna wasanii wengine bila make-up huwaoni ng’o,” alisema Amanda.

No comments