Header Ads

Diamond Ashindwa kuhudhuria Mazishi ya Ivan

 
Kwenye U-heard leo May 30, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametuwekea karibu story inayomuhusu Diamond Platnumz ambaye amekuwa gumzo baada ya kufanya show Nairobi wakati mzazi mwenzake Zari akiwa kwenye msiba wa mume wake wa zamani Ivan.

Gumzo hilo lilienda mbali zaidi kwa madai kuwa Tiffa hajapelekwa msibani kwa sababu baba yake Diamond alimzuia huku story zikihusishwa kuwa Diamond hajahudhuria mazishi kwa sababu amezuiliwa kuingia Uganda hivyo baada ya show ya Kenya alirudi Tanzania.
Soudy Brown alimpigia Diamond lakini hakumpata hivyo alimpigia Meneja wake Salaam kujua ukweli wa mambo haya na alikuwa na majibu haya.
>>>“Ile ilitokea bahati mbaya tukashindwa ku-cancel dakika ya mwisho. Kuna kitu kinaitwa toba, basi tutaomba toba. Kwenye mazishi hatujahudhuria, ilikuwa twende leo Alfajiri lakini sasa kumbe wao wametoka usiku kwenda kijijini. Kwa hiyo nadhani ratiba yetu imeingiliana maana na sisi tulitoka Nairobi jana jioni.”  – Salaam

No comments