Header Ads

FIFA YAJIBU RUFAA YA SIMBA KUHUSU KUIPA POINTI TATU KAGERA, MAJIBU HAYA NI FURAHA KWA WANAYANGA

Habari mpya ni kuwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeijibu barua ya rufaa ya Klabu ya Simba ambayo ilipeleka maombi ya kupinga Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuipa Kagera Sugar pointi tatu.
Katika barua hiyo ya majibu ya FIFA, shirikisho hilo imetupilia mbali maombi ya Simba kupinga uamuzi huo wa TFF kwa Simba, hivyo kwa maana hiyo, Yanga inaendelea kuwa bingwa kutoka na maamuzi hayo ambayo hayatabadili msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom 2016/17.
Ikiwa Simba ingerejeshewa pointi hizo inamaana kuwa yenyewe ndiyo ingekuwa bingwa wa ligi hiyo kwa kuwa Yanga ilitwaa ikiwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa, licha ya timu zote hizo mbili kuwa na pointi sawa.

No comments