Header Ads

Mazishi ya Baba wa Amina Chifupa Leo Kisutu, Dar

KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kapteni Hamisi Chifupa ambaye alikuwa baba wa  aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa (Vijana) wa chama hicho, Amina Chifupa leo alizikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar.

Mzee Chifupa alikutwa na umauti Ijumaa iliyopita majira ya saa mbili usiku baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi uliopelekea kifo chake.

Mazishi ya kada huyo yalihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwan Kikwete na  Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Philip Mangula.

Katika mazishi hayo mjukuu wa marehemu huyo Rahmanino Mpakanjia aliwatia simanzi waombolezaji kwa jinsi alivyokuwa akilia katika hatua mbalimbali za mazishi hayo hasa mwili huo ulipokuwa ukifukiwa.

No comments