Header Ads

Mwanajeshi wa Ghana Auawa na Wananchi Akidhaniwa Jambazi

Kepteni Maxwell Mahama wa Jeshi la Ulinzi la Ghana enzi za uhai wake.
KEPTENI Maxwell Mahama wa Jeshi la Ulinzi la Ghana, Jumatatu iliyiopita aliuawa na wananchi wa eneo la Denkyira-Obuasi kwa kupigwa mawe na kuchomwa moto asubuhi wakati akifanya mazoezi ya kukimbia.
Inasemekana wananchi hao walimwua askari huyo wakidhani ni jambazi kwa kuwa alikuwa na bastola.
Mwili wa Askari huyo ukitolewa kwenye gari.
Waziri wa Ulinzi nchini humo, Dominic Nitiwul, alisema serikali inafanya uchunguzi wa mauaji hayo yanakanganya hususan kwa vile marehemu alikuwa na silaha.

Nitiwul alisema kwamba iwapo watu wengepiga kelele za “mwizi” ni dhahiri angewashambulia kwa risasi kwani angejua atauawa.

“Lakini inaonekana aliuawa kimyakimya bila kupigiwa kelele za mwizi. Au walimvamia bila ya yeye kujua,” alisema waziri huyo.
Waziri wa Ulinzi nchini humo, Dominic Nitiwul.
Waziri huyo ameongeza kwamba jeshi limepeleka maofisa 35 wa kuungana na kundi la upelelezi. Hata hivyo, polisi, wanasema wanashindwa kufanya upelelezi kutokana na kusakamwa na wanajeshi waliojaa huko.

No comments