Header Ads

Pamela Daffa ‘Pam D’ Aogopa Kumuweka wazi mpenzi wakeStaa wa Muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’.

MWANADADA anayefanya vyema kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ amefunguka kuwa anahofia kumwanika mpenzi wake ili kuepuka watu kuwaachanisha kama ilivyo kwa mastaa wengi wanapouanika uhusiano wao.
Akichonga na Mikito Nusunusu, Pam D alisema kuwa amejifunza kutoka kwa mastaa wengi wanaoanika uhusiano wao na kujikuta watu wakiuingilia na kusababisha waachane kwa kuwachonganisha kwa maneno hivyo hataki hilo litokee kwake kwani anampenda kwa dhati mwanaume aliye naye.

“Nipo kwenye uhusiano na mwanaume ambaye ninampenda sana. Sitaki kuachana naye kwa maneno ya watu ndiyo maana nimekuwa nikijitahidi sana kuficha maisha yangu ya uhusiano,” alisema

No comments