Header Ads

SIMBA BINGWA WA FA 2016/17...SIMBA 2-1 MBAO FC UWANJA WA JAMHURI, DODOMA


FULL TIME:
Dakika ya 123: Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inapata ushindi wa mabao 2-1 na kuwa mabingwa wa Kombe la FA.
Dakika ya 121: Mashabiki wa Simba wanashangilia kwa nguvu, Blagnon wa Simba yupo chini baada ya kupigwa kichwani na beki wa Mbao.
Kichuyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa anaipatia Simba bao la pili kwa njia ya penati. Anapiga upande wa kulia kipa anaenda kushoto.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Askari wameingia kuzuia vurugu kutokea uwanja.
Wachezaji wa Mbao wanamvaa mwamuzi wakilalamika kuwa mchezaji wao hakuushika mpira.
PENATIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII Simba wanapata penati.
Dakika ya 118: Presha inazidi kuwa kubwa, Simba wanapata kona.
Dakika ya 115: Simba wanafanya shambulizi kali lakini shuti la Mavugo linagonga nyavu ndogo ya pembeni.
Dakika ya 113: Mchezo sasa umekuwa wa kushambuliana kwa zamu. Mbao wanajipanga vizuri, Simba wasipokuwa makini wataruhusu bao lingine.
Kama ilivyokuwa kwa Mbao, mabeki wa Simba wanafanya uzembe, unapigwa mpira mrefu wanajua mfungaji ameotea, anabaki na kipa kisha anamchambua vizuri, Mbao wanapata bao la kusawazisha.
Ndani Robert anaipatia Mbao bao la kusawazisha.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 108: Simba wamepunguza kasi, Mbao sasa wao ndiyo wanaohaha.
Dakika ya 106: Mshambuliaji wa Mbao, Kotecha anafila langoni mwa Simba lakini mpira unakuwa na kasi unatoka nje.
Dakika ya 105: Mwamuzi anaanzisha mchezo.
Wachezaji wanakunywa maji kisha wanarejea uwanjani kumalizia dakika 15 za nyongeza.
Mwamuzi anapuliza filimbi kumaliza kipindi cha kwanza cha dakika za nyongeza.
Dakika ya 105: Mbao wamefanya mabadiliko ya wachezaji wawili kwa mpigo. Simba wanapata kona.
Dakika ya 102: Mbao wamepunguza kasi, wakiendelea hivi wanaweza kuruhusu bao la pili.
Dakika ya 98: Simba wameongeza kasi ya kushambulia na mashabiki wao wanawashangilia kwa nguvu.
Simba wanapata bao kupitia kwa Balgnon, alipata pasi ndefu kutoka kwa Abdi Banda, beki wa Mbao akafanya uzembe, ikampita, Blagnon akatuliza, akapisha shuti kali na mpira kujaa wavuni.
Dakika ya 96: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO SIMBAAAAAAAAAAAAAAA
Dakika ya 94: Simba wanamiliki mpira tangu kuanza kwa dakika za nyongeza. 
Dakika ya 91: Mchezo unaendelea.
Zimeongezwa dakika 30.
Waamuzi wanazungumza na manahodha katikati ya uwanja huku makocha wakitoa maelekezo kwa wachezaji wao.
Dakika ya 93: Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha pili.
Dakika ya 92: Mbao wanapata faulo karibu na lango la Simba, inapigwa inatoka nje.
Dakika ya 91: Kichuya anapiga shuti kali kipa anapangua inakuwa kona, kona inapigwa kisha mpira unaokolewa, presha ni kubwa.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 89: Kombe limeshawasili uwanjani hapa, limewekwa uwanjani.
Dakika ya 88: Mbao wanajipanga na kuwapa presha Simba.
Dakika ya 87: Simba wanapata faulo karibu na kona, inapigwa na Kichuya lakini mpira unapotea.
Dakika ya 84: Simba wanapata kona, inapigwa inatokea piga nikupige, kona nyingine. Inapigwa Simba wanashambulia inakuwa kona nyingine.
Dakika ya 81: Kipa wa Mbao yupo chini, anavua gloves, mwamuzi anamfuata kumuuliza, baada ya muda anazivaa tena kisha mchezo unaendelea.
Dakika ya 80: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Said Ndemla anaingia Blagnon.
Dakika ya 78: Simba wanapata faulo, inapigwa inatokea piga nikupige lakini kipa anauwahi na kuudaka. Mbao wanajibu mapigo wanafila langoni mwa Simba lakini hakuna bao.
Dakika ya 75: Mchezo ni mgumu kwa pande zote.
Dakika ya 74: Ajibu anapiga pasi ndefu kwa Mavugo lakini anaikosa inatoka.
Dakika ya 73: Mbao wamekuwa na nguvu, sasa wanapanga mashambulizi na kuwapa wakati mgumu Simba. Makocha wa timu zote wamesimama.
Dakika ya 70: Mbao wanarejea tena langoni kwa Simba wakiwa na kasi kubwa. Mbao wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Simba, inapigwa lakini Agyei anaudaka mpira.
Dakika ya 69: Mbao wanalishambulia lango la Simba kwa nguvu, inakuwa kona baada ya mpira kutoka nje, inapigwa lakini inaokolea.
Dakika ya 64: Simba wanapata faulo nje ya eneo la 18 baada ya Jonas Mkude kuchezewa faulo, inapigwa faulo mwamuzi anapuliza filimbi baada ya kipa wa Mbao FC kuchezea wafulo na wachezaji wa Simba wakati wakiwania mpira.
Dakika ya 61: Mbao wanashambulia lakini inakuwa kona kwa Simba, inapigwa lakini Simba wanaokoa.
Dakika ya 60: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Juma Luizio, anaingia bwana  harusi, Ibrahim Ajibu. Mashabiki wa Simba wanashangilia kuona Ajibu anaingia.
Dakika ya 60: Mchezo unaendelea kwa kasi kubwa.
Dakika ya 57: Beki wa Mbao, Kwasi anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Mavufo.
Dakika ya 54: Mbao wanacheza vizuri, wanapiga pasi nzuri, inamfikia Haji anashindwa kumalizia kazi nzuri baada ya kupiga mpira vibaya na unatoka nje.
Dakika ya 51: Simba wanafanya mabadiliko, wanamtoa Mohammed Hussein 'Tshabalala', anaingia Abdi Banda.
Dakika ya 49: Inapigwa kona lakini Simba wanashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 48: Kichuya anapiga mpira kwa nguvu akiuchonga kutoka nje ya 18, unaelekea langoni lakini Ndikumana wa Mbao anaugusa unatoka nje kuwa kona. lilikuwa shambulizi kali.
Dakika ya 48: Mbao wanalikaribia lango la Simba lakini mwamuzi anapuliza filimbi kuwa wameotea.
Dakika ya 47: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye ni mmoja wa wadau waliofika kwenye Uwanja wa Jamhuri kufuatilia mchezo huu. Yupo jukwaa kuu.
Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi kama ilivyo kuwa kipindi cha kwanza.
Timu ndiyo zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.
MAPUMZIKO
Dakika ya 46: Kipindi cha kwanza kimekamilika. Timu zote zinaenda kupumzika.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika moja ya nyongeza.
Dakika ya 43: Mchezaji wa Mbao, Swita anapata kadi ya njano kutokana na kuchezea faulo beki Mohamed Hussein 'Tshabalala'.
Dakika ya 43: Simba wanapiga pasi nyingi lakini hawajafika langoni mwa Mbao kufanya shambulizi kali.
Dakika ya 40: Kasi imepungua kiasi lakini Simba wanaendelea kuwa wenye ngyuvu kutokana na kuumiliki mpira muda mrefu.
Dakika ya 34: Simba wanafanya shambulizi la moto, mkwaju wa Mavugo unamgonga beki, mpira unatoka nje inakuwa kona, inapigwa kona inaokolewa.
Dakika ya 32: Kichuya wa Simba anapiga shuti kutoka nje ya 18 linapaa juu  kabisa ya lango.
Dakika ya 29: Simba wanapata kona. Inapigwa kipa anaudaka mpira.
Dakika ya 28: Mabeki wa Mbao wanafanya makosa, Mavugo anapata nafasi akiwa yeye na kipa upande wa pembeni mwa lango, anapiga shuti kwa nguvu, linapaa juu ya lango.
Dakika ya 27: Mavugo anamchezea faulo kipa wa Mbao wakati wakiwania mpira.
Dakika ya 25: Mbao wanaonekana kuwa vizuri, wachezaji wake wanacheza wakiwa wametulia licha ya presha kubwa.
Dakika ya 22: Timu zote zinashambuliana kwa zamu, mchezo unachezwa katikati ya uwanja muda mwingi.
Dakika ya 20: Kocha wa Simba, Joseph Omog amesimama akitoa maelezo.
Dakika ya 18: Washambuliaji wa Simba wanafika langoni mwa Mbao lakini wanakuwa wameotea.
Dakika ya 16: Mavugo anadhbitiwa na walinzi wawili wakati akikimbilia mpira. Mchezao una kasi kubwa.
Dakika ya 14: Simba wanapata kona, inapigwa lakini kipa wa Mabao anapangua mpira na kuukoa.
Dakika ya 12: Simba wanafika langoni mwa Mbao zaidi ya mara mbili ndani ya muda mfupi, Bukungu anapiga shuti linapaa juu ya lango.
Dakika ya 10: Mavugo anapata nafasi ya wazi, akiwa yeye na kipa anapiga shuti kali lakini linatoka nje ya lango.
Dakika ya 7: Simba wanajibu mashambulizi, wanafika langoni mwa Mbao lakini mwamuzi wanapuliza filimbi kuwa kuna faulo imefanyika.
Dakika ya 4: Mao wanafanya shambulizi kali langoni mwa Simba, linapigwa shuti kali ndani ya 18 mpira unapaa juu, ilikuwa ni baada ya kipa kuupangua mpira.
Dakika ya 2: Mbao wanafika langoni mwa Simba lakini kipa anaudaka mpira.
Dakika ya 1: Mchezo umeanza, presha ni kubwa hapa uwanjani, Uwanja wa Jamhuri umejaa, Simba ndiyo wanaidadi kubwa ya mashabiki uwanjani hapa.
Mwamuzi anaanzisha mchezo. 
Timu zote zimeshaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo huu.
Mchezo wa fainali ya Kombe la FA unapigwa hapa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kati ya Simba dhidi ya Mbao FC.
Timu ambayo itashinda katika mchezo huu itapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuani ya Kombe la Shirikisho. 
Kikosi cha SIMBA ambacho kinaanza katika mchezo huo wa leo hiki hapa:
1.Daniel Agyei  
2.Besala Bukungu 
3.Mohammed TShabalala
4.James Kotei
5.Juuko Murshid 
6.Jonas Mkude
7.Shiza Kichuya
8.Mzamiru Yassin 
9.Laudit Mavugo
10.Said Ndemla 
11.Juma Luizio

Waliopo benchi
1.Dennis Richard 
2.Vincent Costa 
3. Abdi Banda
4.Mwinyi Kazimoto
5. Ibrahim Ajibu 
6.Frederic Blagnon

No comments