Header Ads

Simba Bingwa wa kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) mwaka 2017


Klabu ya Simba Sc imetwaa ubingwa wa kombe la Azam Sport Federation Cup(ASFC) baada ya kuifunga klabu ya Mbao FC, kwa jumla ya mabao 2 kwa 1 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma,

Mchezo huo ulio kuwa wa vuta ni kuvute kwa pande zote mbili umechezwa dakika mia na ishirini baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika na timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana.

Katika dakika selathini za nyongeza klabu ya Simba ilianza kujipatia goli lake la kwanza kuputia mchezaji wa kimataifa Blagnon, dakika 95 ya mchezo, wakati goli la pili la Simba likifungwa na Shiza Ramadhani
Kichuya katika dakika ya 120 kupitia Mkwaju wa Penati baada ya beki wa timu ya Mbao, Juuko kuunawa mpira.

Goli la kufutia machzo la timu ya Mbao limefungwa na mchezaji Ndaki Robertm, kwa matokeo hayo klabu ya Simba inakuwa ya pili kutwaa ubingwa huu toka kuanzishwa kwake baada ya mwaka jana kuchukuliwa na klabu ya Yanga FC .
BY HAMZA FUMO

No comments