Header Ads

SIMBA V MBAO FC NI LEO LAKINI WABUNGE NAO KUTINGA Uwanja wa Jamhuri


Msimu wa 2016/17 unatarajiwa kufikia tamati leo Jumamosi, Mei 27 ambapo Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza zitakutana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma katika fainali mkoani Dodoma.

Timu hizo zinakutana katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup - ASFC 2016/17 ambapo mchezo utaanza saa 10:00 jioni.

Inafahamika kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (2), mshindi wa mchezo wa fainali (Kwa msimu huu kati ya Simba na Mbao), ndiye akayekuwa Bingwa wa Kombe la ASFC, atapewa kombe la ubingwa na zawadi ya fedha kiasi cha shilingi milioni hamisini (50,000,000/-) kama zilivyoainishwa kwenye waraka wa zawadi wa michuano.

Aidha, kabla ya mchezo huo kunatarajiwa kuwa na mchezo wa soka wa utangulizi kati ya Azam Media FC dhidi ya Bunge Sports Club ambayo ni timu ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mchezo ambao unatarajiwa kuanza saa 80:00 mchana.

No comments