Header Ads

Agnes Gerald ‘Masogange’ yamkuta ya supastaa Wema Sepetu

 
DAR ES SALAAM: Siku moja baada ya Agnes Gerald ‘Masogange’ kuondoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi yake kuahirishwa hadi Julai 13, jana supastaa Wema Sepetu, ambaye pia anakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya yalimkuta kama ya Masogange baada ya kesi yake nayo kusogezwa mbele hadi Julai 10, mwaka huu. 
 
Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwampamba kuwa kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini inapaswa kuahirishwa kwa kuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliyepangwa kusikiliza, yuko likizo.

 Februari 4, mwaka huu, Wema na wenzake Angelina Msigwa na Matrida Abas, walikamatwa nyumbani kwake, Kunduchi Ununio jijini Dar wakiwa na dawa za kulevya ambazo ni msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vyenye gramu 1.80.

No comments