Header Ads

AISHI MANULA ASAINI SIMBA KWA SH 50,000,000, MSHAHARA SH 3,000,000Klabu ya Simba imefanikiwa kunasa saini ya Kipa Bora wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017 aliyekuwa akiichezea Azam FC, Aishi Manula na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Aishi Manula ambaye amejifunga kwa miaka miwili Simba , anamfuata aliyekua nahodha wake , John Bocco ambaye tayari ameshatia saini kuwatumikia wekundu wa msimbazi kwa msimu ujao.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza kuwa kipa huyo amesaini kwa dau la shilingi milioni 50, pamoja na mshahara wa shilingi milioni 3.

Katika mkatana wake huo, Manula atakuwa akipewa kimafungu kiasi hicho sha Shilingi milioni 50, ambapo, kwanza atapewa shilingi milioni 25, kisha itafuata milioni 5 na mwisho atamalizia shilingi milioni 20 kabla ya Desemba 15, 2017.

Manula aliondoka Azam FC baada ya klabu hiyo kuwa na mpango wa kubana matumizi huku ikigoma   kutoa pesa za kuwasajili wachezaji wake wanaomaliza mikataba.

Manula amekuwa katika kiwango cha juu katika kipindi cha miaka minne sasa ambapo mbali na kushinda tuzo ya Kipa Bora wa Ligi Kuu mara mbili (2016 na 2017), alikuwa kipa namba mbili Kombe la Kagame mwaka 2015.

No comments