Header Ads

Alichosema Wema Sepetu kuhusu Rayvany na BET zitakazofanyika nchini MarekaniMsanii RayVanny ndiye msanii pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla ambaye anatuwakilisha kwenye tuzo za muziki za BET zitakazofanyika nchini Marekani hivi karibuni. RayVanny amechaguliwa kuwania tuzo ya Viewers Choice Awards ama (Pendekezo la Mashabiki ama watazamaji) na BET wametangaza namna ya kuwapigia kura wasanii ili washinde tuzo hizo.

Pamoja na baadhi ya mastaa kama Elizabeth Michael kumpigia na kumuombea  kura RayVanny kura kwenye kurasa zao za Social media , Wema Sepetu naye ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpigia kura RayVanny kwa kuandika>>>Umechaguliwa tu kuwania lakini kwangu wewe ni mshindi tayari …Unastahili kabisa! V-Vanny Boy. Na haiishii hapa Tuendelee kupiga kura.🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Wasanii wanaowania tuzo ya Viewers Choice Awards pamoja na RayVnanny ni pamoja na  Dave (UK ) Jorja Smith (UK) Amanda Black (South Africa) Changmo (South Korea) Daniel Caesar (Canada) Remi (Australia) Skip Marley (Jamaica)

No comments