Header Ads

Azam Fc Wamsajili Kipa wa Mbao FC ya Mwanza kuwa mbadala wa Aishi Manula


Saa chache baada ya aliyekuwa golikipa wa Azam FC Aishi Manula kutangazwa kuondoka katika club hiyo na kujiunga na club ya Simba, Azam FC usiku wa leo wametangaza mbadala wake.

Azam FC usiku wa kuamkia leo wamemtangaza golikipa Benedict Haule aliyekuwa akiichezea Mbao FC ya Mwanza kuwa mbadala wa Aishi Manula aliyejiunga na Simba, Benedict amesaini mkataba wa miaka miwili.
Benedict Haule akisaini mkataba mbele ya Meneja Mkuu wa Azam FC Abdul Mohammed na Meneja wa timu Philip Alando.
Hii sio mara ya kwanza kwa Benedict Haule kuichezea Azam FC alikuwa akiichezea timu ya vijana ya Azam FC ambapo alikulia katika Academy ya timu hiyo, hivyo kurejea kwake ni sawa na kusema ameamua kurudi nyumbani.

No comments