Header Ads

Chris Brown, Karrueche Ndiyo Basi Tena


KAMA VIPI NIPOTEZEE! Labda ndiyo maneno pekee unayoweza kuyatamka baada ya mwanamuziki mwenye jina kubwa, Chris Brown kuchuniana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Karrueche wakati wa Tuzo za BET zilizofanyika Jumanne nchini Marekani.

Brown alipewa nafasi ya kutumbuiza huku Karrueche akipewa nafasi ya kuwa mtangazaji. Walipotezeanaje? Mchongo wenyewe upo hivi!
Wakati Chris alipokuwa akitumbuiza, Karrueche alikuwa akiondoka kabisa eneo la ukumbi na kwenda sehemu kujificha kama ishara mojawapo ya kutokumuona Chris akiwa jukwaani lakini wakati binti huyo mrembo akitangaza ukumbini, Brown naye alikuwa nyuma ya jukwaa tofauti na wanamuziki wengine ambao hata kama walikuwa na nafasi ya kutumbuiza, bado walikuwa wakila pozi ukumbini wakati kabla ya zamu yao kufika.

Kwa hayo yaliyotokea tu, watu wengi wameweka uhakika kwamba watu hao hawawezi kurudiana tena kwani kama kisingetokea kitu kama hicho, kidogo tungesema kuna chembechembe za kurudiana na kuwa pamoja kama zamani.
Kama hukumbuki, acha nikukumbushe tu kwamba wawili hao waliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda wa miaka mitano mara baada tu ya Chris kutemana na mwanamuziki mwenzake, Rihanna.
(Na Nyemo Chilongani, GPL)

No comments