Header Ads

Dada Yetu Jini Kabula Ameruhusiwa

BAADA ya kuugua wiki kadhaa na kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar akisumbuliwa na matatizo ya afya ya akili baada ya malaria kupanda kichwani, hatimaye staa wa Bongo Muvi, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Akizungumza dada wa Jini Kabula aliyejita-mbulisha kwa jina moja la Dayness alisema kuwa, mdogo wake huyo kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na yupo kwake baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.

“Ameruhusiwa na yupo kwake, mtafuteni muongee naye ila tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri kwa sasa,” alisema dada huyo

No comments