Header Ads

Darassa Kaniandikia Wimbo wa Binadamu - Dogo Janja

Msanii wa muziki hip hop kutoka Tiptop Connection, Dogo Janja.
MSANII  wa muziki hip hop kutoka Tiptop Connection, Dogo Janja,  ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake inayoitwa Utavaaje? amefunguka mengi  juu ya ngoma yake ya kitambo kidogo inayoitwa Binadamu aliyomshirikisha PNC Shino kwamba mwimbaji Darassa amehusika kuandika ngoma hiyo ya Binadamu.
Msanii wa bongo fleva, Darassa.
Darassa ameshiriki sehemu kubwa kwenye ngoma hiyo ambayo Dogo Janja alikuwa katika usimamizi mpya wa Watanashati kwani hata anavyoimba hiyo ngoma ni kama Darassa kabisa.
Alivyoulizwa na Dullah wa kipindi cha Planet Bongo cha kituo cha televisheni cha EATV kuhusu  aliyeiandika ngoma hiyo, alisema  Darassa alihusika kwenye uandishi wake  kwa aslimia 80.

No comments