Header Ads

Halle Berry Anasa Ujauzito Japo Ana Miaka 50

Muigizaji mkongwe, Halle Maria Berry ‘Halle Berry’ (50).

Beverly Hills, Marekani
MUIGIZAJI mkongwe, Halle Maria Berry ‘Halle Berry’ pamoja ya kuwa na umri wa miaka 50 ambao wengi hujikatia tamaa ya kuzaa, amenasa ujauzito na ameweka wazi suala hilo alipohudhuria kwenye hafla huko, Beverly Hills.


Halle tayari ana watoto wawili kwa baba wawili tofauti ambapo mtoto wake wa kwanza, Nahla Ariela Aubry alizaa na Mwanamitindo, Gabriel Aubrey na mtoto wake wa kiume, Robert Martinez amezaa na muigizaji wa filamu, Olivier Martinez.

Mpaka sasa haijajulikana baba wa mtoto huyu wa sasa ni nani kwani hajaliweka wazi hilo, mashabiki wake wamempongeza kwa kuamua kuongeza mtoto huku wakimuombea kujifungua salama.

No comments