Header Ads

INASIKITISHA! Tazama Mazishi ya Mke wa Mzee Yusuf na Alichokisema Makaburini (Video)

Mke wa mzee Yusuf, Marehemu Chiku Hamisi, hatimaye amezikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, shughuli ambayo imehudhuriwa na mamia ya waombolezaji.
Chiku alifariki Jumamosi jioni katika Hospitali ya Amana wakati akijifungua ambapo kichanga kilichokuwa tumboni mwake nacho kilifariki.

Chiku alipoteza maisha akisaidiwa na wauguzi kujifungua kwa njia ya upasuaji ambapo mwanaye aliyekuwa tumboni alifariki pia.

Shughuli za msiba na mazishi zilianzia nyumbani hapo Kariakoo Mtaa wa Amani na Livingstone ambapo mwili ulitolewa nyumbani hapo na kwenda kuswaliwa kwenye msikiti wa Manyema.
Baada ya sala mwili ulipelekwa makaburi ya Kisutu jijini hapa.
Katika mazishi hayo Mzee Yusuf aliishiwa nguvu ambapo aliondolewa makaburini hapo kwa msaada wa waombolezaji.
Mzee Yusuf alikuwa Mkurugenzi wa Bendi ya Jahazi Modern taarab kabla ya baadaye kuamua kuachana na muziki wa kidunia na kumgeukia Mungu wake.

No comments