Header Ads

KOCHA WA MAN U, JOSE MOURINHO ASHIRIKI MAZIKO YA BABA YAKE NCHINI URENO
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho yupo nchini Ureno kwa ajili ya maziko ya baba yake mzazi ambaye amezikwa leo Jumanne.
Mzee huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 79 baada ya kuugua kwa miezi kadhaa.

Baba huyo, Jose Manuel Mourinho Felix, alifariki Jumapili iliyopita na atakumbukwa kwa kucheza soka katika timu za Vitoria Setubal pamoja na timu ya taifa ya Ureno aliyoichezea mechi 274 kati ya mwaka 1955 hadi 1974.

Baada ya kustaafu, alipata ajira ya kuwa kocha katika timu kadhaa zikiwemo Uniao Leiria, Amora, Rio Ave, Belenenses na Vitoria.
Leo amezikwa mjini Setubal nchini Ureno na Mourinho amesafiri kutoka Manchester, England hadi Ureno kushiriki mazishi.

Mourinho aliungana na mkewe na watoto wake wawili kushiriki mazishi ya Felix.

No comments