Header Ads

Lwandamina Amtumia Ujumbe Mzito Ngoma

Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina.
KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, ametuma ujumbe mzito ulioambatana na pongezi kwa Mzimbabwe, Donald Ngoma mara baada ya kupata taarifa za nyota huyo kuongeza mkataba.
Ujumbe huo, aliutoa mara baada ya kupata taarifa za mshambuliaji huyo kukubali kuzuia jaribio la Simba iliyokuwa inamuwaniwa vikali kwa ajili ya kumsajili katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mzimbawe huyo, juzi Jumatano alikubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuichezea timu baada ya mkataba wa awali kumalizika.

Lwandamina alituma ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Facebook akimpongeza mshambuliaji huyo kwa maamuzi makubwa aliyoyachukua ya kukubali kubaki kuendelea kuichezea Yanga kwenye msimu ujao.
Ujumbe huo alioutoa Lwandamina huenda likawa dongo kwa kiungo mchezaji raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima anayetajwa kusaini mkataba Simba.
Lwandamina aliandika hivi: “Siyo kitu kigumu kufanya maamuzi pale unapotambua thamani yako.
“Nakupongeza Ngoma kwa maamuzi hayo uliyoyachukua, Ngoma ‘Good Boy’.”
Kocha huyo anatarajia kurudi nchini mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu ujao
Stori: Wilbert Molandi | Championi Ijumaa

No comments