Header Ads

Man United Yaachana na Zlatan Ibrahimovic
Club ya Man United ya England msimu uliyopita ilimsajili staa wa soka wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kama mchezaji huru kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya staa huyo kumaliza mkataba na club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Zlatan alikuwa anatajwa kwa kiasi kikubwa kuwa mkataba wake uliyokuwa unamalizika mwisho wa msimu huu na Man United, angeongezewa wa mwaka mmoja zaidi lakini kuumia kwake kumeifanya Man United kutangaza maamuzi ya kuachana nae.

Ibrahimovic aliumia goti mwezi April wakati wa mchezo wa Europa League na baada ya kufanyiwa uchunguzi iliripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja hadi mwaka 2018, hivyo kumalizika kwa mkataba wake kumeifanya Man United kuamua kuachana nae jumla.

No comments