Header Ads

MAN UNITED YAKAMILISHA USAJILI WA JEMBE KUTOKA KWAO ZLATAN IBRAHIMOVIC KWA PAUNI MILIONI 31

Manchester United wamefikia makubaliano ya kumsaini beki raia wa Sweden Victor Lindelof kutoka Benfica kwa kima cha pauni milioni 31.


Man United wanasema kuwa kilichobakia ni makubaliano ya kibinafsi na uchunguzi wa kiafya ambavyo viitafanyika wiki ijayo.

Lindelof ambaye ameichezea nchi yake mara 12 anatarajiwa kushiriki mechi ya kirafiki nchini Norway siku ya Jumanne. Anatokea taifa moja na straika mkongwe Zlatan Ibrahimovic.

Mchezaji huyo mwenye miaka 22 ambaye amekuwa akiichezea Benfica tangu mwaka 2012 atakuwa mchezaji wa kwanza kusainiwa na Man U msimu huu.
Lindelof alicheza mara 47 klabu hiyo ya Ureno msimu uliopita.

Victor Jörgen Nilsson Lindelöf
Kuzaliwa: Julai 17, 1994 (miaka 22)
Alipozaliwa:  Västerås, Sweden
Urefu: Futi 6 inchi 2
Nafasi: Beki wa kati

Klabu alizocheza
2009–2012     Västerås SK
2012–     Benfica B     96
2013–     Benfica

Timu za taifa
2010–2011     Sweden U17     5
2012–2013     Sweden U19     17
2014–2015     Sweden U21     13
2016–     Sweden     12

No comments