Header Ads

MASHABIKI WALE WA SIMBA, OKWI HUYU HAPA, YUPO NA HANS POPPE, HAJI MANARA ASEMA DILI LIMETIKI
Mshambuliaji Ibrahim Ajib yupo njiani kuelekea Yanga akitokea Simba, hiyo siyo habari nzuri kwa Wanasimba lakini kuna taarifa njema kwao.

Habari kutoka ndani ya Klabu ya Simba inaeleza kuwa klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za kumvalisha Emmannuel Okwi jezi namba 25 ambayo alikuwa kiitumia kikosini hapo kama usajili wake utakamilika.

Okwi ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, inadaiwa kuwa alitua jijini Dar es Salaam, jana usiku yupo katika mazungumzo ya mwishomwisho na klabu hiyo.

Kupitis ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ambaye alikuwa Ofisa Habari wa Simba, ameweka picha ya Okwi akiwa na Mwenyeki wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kisha kuandika ‘DEAL DONE’, ikionekana anamaanisha kila kitu kimekamilika.

No comments