Header Ads

Maua Sama Anapenda kuwa kwenye uhusiano na WazunguMwanadada anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Maua Sama.


BAADA ya tetesi kuzagaa kuwa ameopoa pedeshee wa Kizungu, mwanadada anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Maua Sama ameibuka na kufungukia ishu hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo kilichopo karibu na msanii huyo, kililitonya Risasi Vibes kuwa, Maua hapendi kuweka uhusiano wake wazi kwa sasa anabanjuka na Mzungu ambaye ndiye anayemuweka mjini kwa asilimia kubwa na mara nyingi anapenda kuwa kwenye uhusiano na Wazungu  kwani anawapenda sana.

Baada ya kuinyaka ishu hiyo, Risasi Vibes ilimtafuta Maua aliyefunguka huku akiangua kicheko; “Haahaaa, jamani hayo ni mambo yangu binafsi sitaki kuongelea, ishu za uhusiano wangu sipendi kuzianika hadharani, tuzungumzie masuala ya kazi yangu ya muziki.”
 Stori: Mayasa Mariwata | Risasi Mchanganyiko | Risasi Vibes

No comments