Header Ads

Maunda Zorro ‘Abaniwa’ Na Familia! Kwa sasa Analea watoto

Mwanamuziki mwenye sauti ya ‘kusahaulisha kero za baba mwenye nyumba’, Maunda Zorro.
 MWANAMUZIKI mwenye sauti ya ‘kusahaulisha kero za baba mwenye nyumba’, Maunda Zorro amesema sababu mojawapo inayomfanya asisikike kwenye anga la Bongo Fleva ni pamoja na malezi kwa familia yake, ambayo ni watoto na mumewe huku akiweka wazi kuwa kuimba hakulazimishwi na mtu hivyo hata anapoacha kufanya hivyo hakuna wa kumuuliza na kumsumbua.

Akichonga na Star Mix, Maunda aliyewahi kubamba na Wimbo wa Mapenzi ya Wawili alisema; “Kwa sasa nalea watoto na pia mume wangu anahitaji muda wangu mwingi, hivyo unakuta nashindwa kujigawa kwa namna ambavyo watu wanataka lakini Inshallah Mungu akijaalia nitaimba tena, ingawa siwezi kuhakikisha kwa asilimia zote,” alisema Maunda

No comments