Header Ads

Michael Wambura Achukua Fomu Ya Kuwania Makamu Rais Wa Tff


Michael Richard Wambura amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF).
Wambura ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara amejitokeza leo kwenye ofisi za TFF mitaa ya Karume jijini Dar e Salaam.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Wambura alisema nafasi ya Makamu wa Rais siyo ndogo na hata katika uchaguzi uliopita aligombea nafasi hiyo, hivyo ameona ni jambo la busara kuendelea pale alipoishia.

Amesema kugombea kwake nafasi hiyo hakumaanishi aliyepo katika nafasi hiyo hafai, bali yeye ataanzia pale alipoishia mwenzake kama atapata nafasi.

Kuhusu atafanya nini akiingia madarakani amesema kuwa hilo ni suala la kampeni na ataanza kulizungumza muda sahihi utakapofika.

No comments